PICHA TOKA MAKTABA
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia zinasema kuwa katika ajari ya kwanza, lori la mizigo (semi trailer) lilimgonga muendesha baiskeli aliyekuwa akipita kandokando ya barabara na kumuumiza vibaya hali iliyopelekea kupoteza maisha palepale.
Wakati askali wa usalama barabarani akiendelea kupima ajari hiyo na watu wakiendelea kukusanyika kwa lengo la kushuhudia au kuangalia kama aliyegongwa wanamfahamu na kuweza kutoa msaada, ndipo lilipokuja basi mali ya kampuni ya mabasi ya SUMRY lililokuwa likitokea mkoani kigoma kuelekea jijini Dar es salaam kwa mwendo wa kasi bila dereva kujua kilichokuwa kinaendelea barabarani na kwagonga watu kumi na tatu akiwemo na askali wa usalama barabarani aliyekuwa akipima ajari ya kwanza na kuwasababishia vifo watu wote kumi na tatu palepale.
Baada ya kuona hivyo,dereva wa basi hilo la SUMRY aliamua kuendelea na safari hadi alipofika kituo cha polisi mkoani Singida na kujisalimisha.
Hadi taarifa hizi zinatufikia,miili ya marehemu wote ilikuwa njiani kupelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa mkoa wa Singida pamoja majeruhi katika ajari hiyo.