AJALI!!! BASI LA KAMPUNI YA HAI LAUA MWENDESHA PIKIPIKI MJINI MOSHI!!



Basi la kampuni ya HAI EXPRESS lenye namba za usajiliT439 BYS lililokuwa likitokea jijini Dar es salaam kuelekea jijini Arusha, limemgonga na kumsababishia umauti mwendesha pikipiki mmoja mkoani Kilimanjaro wilaya ya Moshi. Mashuhuda wa ajali hiyo wametudokeza kuwa, ajali hiyo imetokea wakati basi hilo la HAI EXPRESS likielekea standi kuu ya mabasi mkoani humo.

Baada ya tukio hilo, dereva wa basi hakusimama eneo la tukio kuhofia usalama wake kwa sababu waendesha pikipiki wengi maarufu kama bodaboda walikuwa wakimfuata kwa hasira kuashiria kutaka kumpiga kwa kusababisha kifo cha mwenzao, taarifa zinaendelea kubainisha kuwa , dereva huyo aliyekuwa akiendesha basi, alishawahi kuhusika katika ajali ya basi la NGORIKA iliyosababisha vifo pia na kupelekea leseni yake kufungiwa.

WASAFIRI TANZANIA MEDIA tunaiomba mamlaka husika kulifuatilia hili na ikibainika basi mmiliki wa basi achukuliwe hatua kali kwa kuendelea kutumia madereva wenye kifungo cha leseni huku akiwa anafahamu.








Previous
Next Post »