IBRA LINE YATANGAZA NAULI MPYA KWA MABASI YAKE,ABIRIA SASA KULIPA NUSU BEI YA SUMATRA.......!


SIKU chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kutangaza punguzo la bei ya Mafuta Kampuni ya kutoa huduma ya usafirishaji wa ndani na nje ya nchi, Kampuni ya mabasi ya  IBRA LINE imetangaza kushusha nauli kwa nusu ya bei elekezi ya SUMATRA kwa safari zake zote.

Hatua hiyo inakuja wakati baadhi ya wananchi wakilalamika kutokuwepo na ahueni yoyote licha ya kwamba serikali imetangaza kushusha bei ya bidhaa ya Mafuta kwa nchi nzima kufuatia  bidhaa hiyo kushuka bei katika soko la dunia.
Akizungumza ofisini kwake mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ibrahimu Shayo alisema Kampuni yake imefikia hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa wateja wake ambao wamekuwa wakitumia huduma ya usafiri inayotolewa na kampuni yake ya IBRA LINE kila siku.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibraline ,Ibrahim Shayo.

“Tumeamua kufanya hivi lengo likiwa ni kuwashukuru wateja wetu wanao tumia huduma ya usafiri unaotolewa na kampuni yetu ya Ibraline…ningewajua mmoja mmoja ningeweza kuwapa mkono lakini kwa kuwa wanaishi maeneo tofauti ndio sababu tumeamua kurudisha kile tunachopata kwa njia ya kuwapunguzia bei.”alisema Shayo.


Previous
Next Post »