Mamlaka ya udhibiti wa usafirishaji nchini SUMATRA, imeyafungia mabasi ya kampuni ya usafirishaji abiria nchini ya PRINCES MURO kutoendelea na utoaji huduma ya usafiri kati ya mikoa ya ARUSHA na DAR ES SALAAM, DAR ESALAAM na MWANZA kutokana na kukiuka sheria ya usafirishaji n usalama barabarani. Uamuzi huo umefikiwa na malaka hiyo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa abiria juu ya ubovu wa huduma zitolewazo na kampuni hiyo.
Katika barua ya SUMATRA inasema kuwa, moja ya mabasi ya kampuni ya muro ilikuwa ikitokea Da es salaam kuelekea Arusha na lilipofika chalinze liliharibika na kukaa hapo bila marekebisho wala taarifa au msaada wowote kwa abiria hadi kufikia saa sita usiku na bila kuwapatia abiria msaada wowote wa kibinadamu.
Pia barua hiyo ilielezea kuwa malalamiko yalizidi kupokelewa juu ya mabasi ya kampuni hiyo kwa njia za mwanza na arusha kuendelea kuharibika katika maeneo mbalimbali kama vile RUVU darajani, Maili moja na Chalinze kwa nyakati tofauti tofauti.
Kwa ukiukwaji huo wa kanuni namba 21 na 22 ya leseni ya usafirishaji wa abiria ya mwaka 2007, na kanuni namba 11(1)(b) ya viwango vya ubora na usalama ya mwaka 2008, SUMATRA imefikia uamuzi huo wa kuyafungia mabasi hayo na kumtaka mmiliki wake ambaye ni MURO INVESTIMENT kuyafanyia matengenezo na kufanyiwa ukaguzi na mkaguzi kutoka jeshi la polisi kikosi cha usalama ili kuhakikisha yanakidhi viwango vya usalama na ubora.