Taarifa za awali zilizoifikia WASAFIRI BLOG, zinasema kuwa watoa huduma hao wameamua kupanua wigo wa huduma zao kwa lengo la kuweza kuwafikia watu wengi na kuwapunguzia uchovu wa kutumia siku mbili katika safari kwa kutoka Chunya na kulala Mbeya kisha kuondoka kesho yake kwa safari ya Dar es salaam.
Na kuhakikisha hilo kampuni hizo zimeshatoa basi Mmbili mbili kila moja kwa ajili ya kuanza safari kwa njia hiyo.
Uboreshaji wa barabara ya Chuny hadi Mbeya kwa kiwango cha lami kumechangia kiwango kikubwa kuondoa kero ya usafiri ambayo imekuwako kwa muda mrefu baina ya wilaya hiyo na mkoani. Hivyo kuboreshwa huko kunaonekana kuzidi kuwahamasisha watu mbalimbali wakiwamo wawekezaji kuzidi kumiminika katika wilaya ya chunya kwa ajili ya kufanya uwekezaji, na RUNGWE NA JM LUXURY ni mwanzo tuu kwani tuna tumaini watafuata wengi sana.