WATU 22 WAFARIKI NA WENGINE ZAIDI YA 30 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI MKOANI IRINGA!!!!!!



Watu 22 wameripotiwa kufariki dunia na wengine 34 kujeruhiwa katika ajali ya basi kampuni ya Another G lililokuwa likitokea mkoani Iringa kuelekea mkoani Njombe. Ajali hiyo ilihusisha basi hilo mali ya kampuni ya Another G likitokea mkoani Iringa kuelekea mjini Njombe kugongana uso kwa uso na lori la mizigo (SEMI TRAILER) lililokuwa limebeba shehena ya madini ya shaba katika wilaya ya Mafinga maeneo ya Kinyanambo njia panda ya Madibila.

Kati ya watu 22 waliofariki, 15 ni wanaume na wengine 7 ni wanawake na miili yao imeshapelekwa katika hospitali ya Mafinga, kwa taarifa za haraka zinasema kuwa madereva wote wawili wamefariki.




TUTAENDELEA KUWAJUZA ZAIDI KADILI TUTAKAVYOKUWA TUNAPATA TAARIFA ZAIDI JUU YA TUKIO HILI.

Previous
Next Post »