AJARI!! BASI LA RATCO LAPATA AJARI MJINI KIBAHA!!!

Hili ndiyo basi mali a kampuni ya RATCO EXPRESS ya mkoani Tanga linalofanya safari kati ya mikoa ya Tanga na Dar es salaam lililopata ajari mjini kibaha mkoani Pwani katika eneo linaloitwa Kongowe.

Kwa mujibu wa maelezo ya shuhuda wetu, ambaye pia ni mmoja kati ya wafanyakazi wa kampuni ya RATCO katika basi hilo,ameweka mezani taarifa kuwa ajari hiyo ilisababishwa na mwendo kasi wa gari dogo lililokuwa mbele yao uliopelekea gari  hilo dogo kuchomoka tairi na ndiyo basi lao kwenda kulikanyaga tairi hilo na kupoteza muelekeo na kupindukia upande wa kushoto wa barabara.

Hadi tunaenda mitamboni taarifa tulizokuwa nazo ni kuwa hakuna mtu aliyekufa ila ni majeruhi madogo madogo ya michubuko na kukatwa na vipande vya chupa zilizotokana na kupasuka kwa vioo vya gari.

TAZAMA BAADHI YA PICHA ZA AJARI.
Baadhi ya abiria wakihangaika kujinasua katika basi hilo kwa kila namna kama wanavyoonekana hapa



Previous
Next Post »