Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mabasi mapya yaendayo kasi ya ajabu
yliyoshushwa na kampuni ya Shabiby Line yamezidi kuwa gumzo kutokana na
wananchi wengi kuyakimbilia huku wakiponda mabasi mengine.
Habari
toka Mkoani Dodoma ndiko makao makuu ya kampuni hiyo ukiacha Gairo
zinasema kuwa wananchi wengi kwa sasa wamekuwa wakitaka kupanda mabasi
hayo kwa ajili ya kujihakikishia usalama wao na kila siku ya mungu
mabasi hayo hujaa siti zake mapema.
Akiongea
na Bossngasa.com meneja wa Kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la
Saidi alisema" Dada unajua haya mabasi ni mapya hivyo wananchi wengi
wanahitaji kusafiri salama na haraka hivyo kwa siku mabasi yote hujaa
hali inayowafanya abiria kubuku safari siku mbili kabla kwa kuhofu
kukosa nafasi ndani mabasi hayo" Alisema
Hata
hivyo pongezi za dhati zimfikie Mbgunge wa Jimbo la Gairo Mh' Ahmed
Shabiby kwa kuonesha upendo kwa watanzania kwa kuwaondolea adha za
usafiri kwani mabasi hayo mapya 26 yameanza safari wiki iliyopita na
lengo lake ni kabla ya mwaka huu kumalizika atashusha mengine kama haya
kwa ajili kukidhi haja ya usafiri mikoa yote Tanzania.
HAPA MOJA YA BASI HILO LIKIWA KWENYE KITUO CHA MAFUTA CHA SHABIBY MKOANI DODOMA WIKI ILIYOPITA KABLA YA KUANZA SAFARI
HAPA BASI HIZO KWA NDANI KAMA ZINAVYOONEKANA
VYOO VILIVYOMO NDANI YA MABASI HAYO YA MWENDO KASI NCHINI
MABASI HAYO YAKIWA YAMEJIPANGA KWENYE YADI YA SHABIBY DODOMA MJINI KWA HATUA ZA MWISHO KABLA YA KUANZA SAFARI ZAKE.
MWANDISHI HUYO AKIPIGA PICHA KAMA KUMBUKUMBU NDANI YA MABASI HAYO YA KISASA.
SOURCE: BOSINGASA.BLOGSPOT