HII NDIYO MELI KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI,NI MARA TANO ZAIDI YA TITANIC!!!!!!!!


OASIS OF THE SEA ndiyo meli inayosadikiwa kuwa ni kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani kwani ukubwa wake ni mara tano zaidi ya ile ya TITANIC iliyokuwa ikiaminika kuwa ndiyo meli kubwa kuliko zote duniani. Utengenezaji wake umegharimu kiasi cha dola za kimarekani bilioni $1.5.

Imetolewa oda na kuanza kutengenezwa tarehe 12/11/2007 na kukamilika tarehe 28/10/2009 na kukabidhiwa tarehe kwa ajiri ya kuanza kazi tarehe 5/12/2009.

Oasis of the seas ina urefu wa mita 361.6 sawa na futi 1186.5, ina kimo cha urefu wa mita 72 sawa na futi 236 ambayo ni sawa ghorofa ya rosheni 20 kwenda juu, upana wake ni mita 47 sawa na futi 154.

Ina jumla ya engine 8 aina ya wartsila V12 zenye uwezo wa 17500hp.ina lifeboats 18 ambazo zina uwezo wa kuchukua watu 370 kila moja na meli yenyewe ina uwezo wa kuchukua abiria 6000.

Ina ngazi 16 zenye vyumba vya kulala, ina restaurant, ina maduka,hotel za high class,swimming pool, mandhari yenye miti ya kupumzikia, kumbi za disko,michezo ya kwenye maji na mambo mengi.

HIYO NI KWA UFUPI TUU,ZAIDI TEMBELEA
 www.ship-technology.com/projects/oasisoftheseas/
 http://en.wikipedia.org/wiki/MS_Oasis_of_the_Seas
 http://twistedsifter.com/2009/11/oasis-of-the-seas-worlds-largest-cruise-ship/.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
 





















Previous
Next Post »