TUKIO LA NYUMA!!! BASI LA HAI EXPRESS LILIPOPATA AJALI MKOANI IRINGA

 
 
Na Francis Godwin
ABIRIA zaidi ya 40 waliokuwa wakisafiri na  basi la kampuni ya  Hai Express lenye namba  za usajili  T 618 DNI Nissan kutoka  mkoani Mbeya kwenda Dar es Salaam wamenusurika kifo baada ya dereva  basi hilo kushindwa  kulimundu basi lake na  kuligonga lori ambalo likiwa mbele na costa ya Another G iliyokuwa  ikielekea 
Njombe.  

Ajali  hiyo  imetokea  mida ya saa 4.50 asubuhi  eneo la Njiapanda ya Tosamanganga katika barabara  kuu ya Iringa -Mbeya  wakati basi hilo likielekea jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza na mwanahabari wetu eneo la tukio abiria  walionusurika katika ajali  hiyo  walisema kuwa chanzo cha ajali  hiyo  dereva  wa basi  hilo kulazimisha kulipita  lori lililokuwa mbele na hivyo kushindwa kupita baada ya kutokea Costa  yenye namba  T 885 BNQ mbele na hivyo kulazimika kupenya katikati ya lori na  Costa hiyo ya Another G kabla ya kuligonga  lori hilo katika tela lake  upande wa kushoto.

John Kyando ni mmoja kati ya abiria  wa basi hilo la Hai aliyekuwa akitokea mkoani Mbeya kwenda Morogoro  alisema  kuwa  dereva  wa basi hilo alionyesha uzembe wa hali ya  juu  kutokana na kutaka  kulipita  lori  lililokuwa  mbele yake  huku mbele  yake kukiwa na Costa  hiyo ambayo tayari ilikuwa  imesogea jirani na lori hilo.

Alisema  kuwa dereva wa basi hilo baada ya kuona costa  hiyo  imesogea jirani ili  kuepusha kugongana uso kwa uso na Costa  hiyo ndipo alipolazimika  kulikwepesha basi hilo pembeni na kulivaa Lori hilo upande wa tela na kupelekea  basi hilo kuharibika  vibaya upande wa kushoto kwa dereva na baadhi ya abiria  kupata  michubuko kiasi .

Hata  hivyo kwa upande wake Anna Kibiki  alishauri  kuwa  ni vema madereva wa mabasi makubwa  kuwa makini zaidi pindi  wanapokuwa barabarani na kudai  kuwa tatizo la basi hilo la Hai ni  hitilafu za breki kwani  toka  basi hilo  linalotoka Mbeya Dereva  alisikika akilalamikia break kutofanya kazi vema.
 
Alisema bila kutumia mbinu ya  kuligonga  lori hilo yawezekana abiria waliokuwemo katika basi hilo wamepatwa na madhara makubwa  zaidi .
 
 
Abiria  wa basi la Hai Express lenye namba za usajili T 618  DNI waliokuwa  wakisafiri  kutoka Mbeya kwenda Dar es Salaam wakiwa  wamekwama eneo la Njiapanda ya Tosamaganga kwenye barabara  kuu ya Iringa -Dar es Salaam baada ya basi hilo kupata ajali kwa  kuligonga lori lililokuwa mbele yake jana


source na: http://eddymoblaze.blogspot.com

Previous
Next Post »