BREAKIG NEWS!!! WADAU WA USAFIRI SEHEMU MBALIMBALI WATOA DUKUDUKU KWA KAMPUNI YA HOOD LIMITED!!!!!


Wadau mbalimbali wa usafiri kutoka katika mikoa mbalimbali wametoa madukuduku yao yanayohusu usafiri kwa kampuni yao waliyoizoea ya HOOD BUS COMPANY LIMITED yenye maskani yake mtaa wa  mtawala mkoani Morogoro wametoa madukuduku yao kuwa kampuni hiyo inatakiwa ilete mabasi mapya kwa ajiri ya abiria wake kwani wamekuwa wakipata shida sana wanapotumia usafiri wa kampuni hiyo kwa mabasi hayo kuharibikaharibika njiani na kuwapa kero zisizokuwa za lazima abiria wake.
 Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa njia ya simu kutoka mikoa mbalimbali waliokumbwa na dhahama hiyo na kuamua kutoa madukuduku yao, bwana David Kamana akiwa Mwanza ameksema ya kuwa kwa kipindi kifupi tumeshuhudia ajari kadhaa za mabasi ya kampuni hiyo zikisababishwa na uchakavu wa vyombo hivyo,aliendelea kusema kuwa amekuwaa akipata usumbufu wa mara kwa mara pindi akiwa anaelekea kazini kwake kwa basi la kampuni hiyo wilayani kilombero kwa kuharibika kwa mara kwa mara kwa basi.

Bwana Joseph Machange wa mjini Moshi amesma kuwa basi hizi kwa sasa zimeshachoka kwani zimetumika muda mrefu sana na zaidi ya mara tatu wampetwa na dhahama ya kuharibikiwa na basi la kampuni hiyo wakiwa njiani kuelekea jijini Mbeya na wakirudi Moshi pia.Wadau zaidi wamekuwa na maoni kuwa kwa sasa ni wakati wa kampuni ya hood kuwakumbuka abiria wake kwa kuwapatia kitu ile roho inapenda.

Wamekazia kwa kusema kuwa kampuni ya HOOD ni kampuni ya muda mrefu katika sekta ya usafiri nchini na imejibebea wapenzi wengi ambao wanaiamini hadi hivi sasa na kumuomba mmiliki wa kampuni hiyo ndugu HOOD kuwaletea basi mpya na za kisasa kama wamiliki wengine wanavyofanya!

TAZAMA PICHA ZA MABASI YA HOOD HAPA CHINI!





















Previous
Next Post »