Kampuni ya usafirishaji wa abiria katika mikoa ya kanda ya ziwa pwani na kati ya SUPER SAMI EXPRESS jana imeadhimisha miaka mnne tokea imeanza kutoa huduma za usafirishaji wa abiria na vifurushi kwa mikoa ya kanda ya ziwa na mkoa wa Dar es salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bwana JOSIAH MZURI amesema kuwa anamshukuru mungu kwa kufikia hatua hiyo na kuendelea kumuomba Mungu kuzidi kutia baraka zake katika kazi yake hiyo na kufikia hadhi za juu ambapo itakuwa ni kuhudumia taifa zima kwa huduma bora na za kukidhi mahitaji ya abiria.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa,hapo awali wakati kampuni ya SUPER SAMI inaanza kutoa huduma 2012 ilianza ikiwa na basi moja lililotengenezwa na Choda Fabricators nchini Kenya, lakini kwa sasa kampuni ina zaidi ya mabasi nane ambayo manne ni kutoka ZHONG TONG China
Pia kampuni hiyo imekuwa ikitumia pia mabasi kutoka kampuni ya YUTONG China kwa ajiri ya kusaidia kutoa huduma za usafiri katika mikoa mbalimbali kulingana na ruti husika.
Kampuni hiyo imekuwa na mafanikio kiasi cha kuweza kupanua wigo wa huduma zake kutoka safari moja tu ilipokuwa inaanza mwaka 2012 na sasa kuwa na ruti zinazofikia nne mwaka 2013-14 ambazo ni
MWANZA-DAR ES SALAAM
MWANZA-DODOMA-IRINGA
MWANZA-BUKOBA
MUSOMA-MWANZA-DODOMA
HAPPY BIRTHDAY SUPER SAMMY!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!