MWANADADA NA DEREVA WA KIKE WA MABASI YA MIKOANI AHAMIA NDENJELA....!!!!!!!!!!!!!



Mwanadada Nusra Maguluko aliyekuwa gumzo katika sekta ya usafirishaji wa abiria kwa mabasi makubwa nchini Tanzania akiwa na kampuni ya mabasi ya SHABIBY LINE,akiendesha basi la SHABIBY LINE lililokuwa likifanya safari zake katka mikoa ya Dodoma na Dar es salaam.

 Picha juu; Nusra maguluko akiwa kazini enzi akiwa na basi la kampuni ya SHABIBY LINE (DODOMA-DAR ES SALAAM)

 Basi alilokuwa akiliendesha Nusra Maguluko wakati alipokuwa SHABIBY LINE


Kwa sasa amebadirisha route kwenda kufanya kazi katika ruti mpya kwake kati ya mikoa ya Dar es salaam na Mbeya akiwa na basi la NDENJELA EXPRESS akiwa na baadhi ya wafanya kazi wenzake wa kike kama yeye!.

Nusra Mguluko aliyevaa full suit wa pili kutoka kulia akiwa kaika picha ya pamoja na wenzake kabla ya kuanza safari yake
 Nusra akimkabidhi mwenyezi Mungu safari yake kwa maombi kabla ya kuanza safari.
 Mwanadada Nusra Maguluko akiondoa gari stendi Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam baada ya kuhakikisha abiria wake wako sawa.
 Kondakta wa basi la mwanadada Nusra akiwa anafanya tathmini ya abiria wake baada kuanza safari yao ya kuelekea jijini Dar es salaam.
 Hawa ni abiria waliokuwa wakifurahia uendeshaji wa mwanadada Nusra kwani hapo awali walikuwa hawaamini kama mwanadada huyu angeweza kumudu kuendesha basi la abiria kwa umbali huo.
 Hili ndiyo basi analoliendesha mwanadada Nusra Maguluko na hapa alisimama kwa ajiri ya abiria wake kupata nafasi ya kuchimba dawa na kupunga hewa!
 Basi la mwanadada Nusra Maguluko likiwa lina chanja mbuga kuelekea jijini Dar.

TIMU NZIMA YA TANZANIA BOUND BUSES BLOGSPOT TUNAAMINI KUWA WAPO WAKINA DADA WENGI WENYE UWEZO KAMA WA NUSRA ILA WANAOGOPA KWA KUHOFIA MAMBO MBALI MBALI IKIWA NI PAMOJA NA KUWA NA IMANI KUWA UDEREVA WA MABASI NI KWA AJIRI YA WANAUME TUU NA WANAWAKE NI KWA KAZI NYINGINE! JITOKEZENI KWANI JAMII INAWAHITAJI SANA JAMANI,MWENZENU AMEKUWA NI CHANGAMOTO.


Tunajiandaa kuwaletea Historia yake tokea alipoanzia na Hadi leo yuko hapo.

Previous
Next Post »