KAMPUNI YA SHABIBI YAINGIZA MABASI MAPYA!!!!!!!


Kampuni ya mabasi ya SHABIBY LINE yenye maskani yake wilaya ya Gairo mkoani Morogoro inatarajia kuleta mabasi mapya na ya kisasa nchini kwa lengo la kutoa huduma za usafiri kaika mikoa mbalimbali ya nchini Tanzania.
Taarifa zilizotufikia TANZANIA BOUND BUSES BLOGSPOT zinaweka bayana kuwa basi hizo ambazo kwa sasa ziko njiani kuja nchini  kwa idadi zinakadiriwa kuwa ni kumi na sita.

 Basi hizo ambazo zimetengenezwa na ku dizainiwa na kampuni ya YUTONG iliyopo nchini China ni tofauti kabisa na mabasi mengine yaaliyokwisha kutolewa na kampuni hiyo kutoka china na kwamba kampuni ya SHABIBY LINE ndiyo itakuwa kampuni ya kwanza barani Afrika kuingiza na kutumia aina hii ya mabasi ya YUTONG.

Mabasi hayo ambayo yametengenezwa kumudu mazingira na hali ya hewa ya Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa hiyo hayatakuwa na usumbufu na matatizo kama mabasi ya awali ya kampuni hiyo!  









Previous
Next Post »