SAFARI YETU YA MBEYA KWENDA DODOMA NA BASI LA SKY LINE ILIKUWA HIVI......!!!!

Tuliondoka jijini Mbeya majira ya saa kumi na mbili kamili alfajiri, nikipandia basi kituo kinachoitwa Ilomba, tulipokuwa ilomba gari ya kwanza kupita ilikuwa ni Meya express ya Mbeya to Arusha ambayo ilipita saa kumi nambili kasoro dk tano ikafuata gari yetu baade ikafuata HOOD ya Mbeya to Arusha.



Tumeingia makambako ilikuwa majira ya saa mbili na dakika tano tulikuwa tumeshaingia makambako stendi na hatukukaa kwani tuliingia tuu na kutoka .


Tulipofika mizani,nyuma yetu tayari alikuwa ABOOD BUS ya Mbeya TO Dar es salaam namba T297ATH.,Tulipima na kuondoka kuelekea sehemu moja ambayo ni maalumu kwa ajiri ya kuchimba dawa ni maarufu kwa jina la CHIMBA DAWA! Hapo tulikuta basi la HAPPY NATION likiwa limeshafika, na baada ya hapo aliingia ABOOD,kiwa amefuatana na HOOD ya Arusha, kisha NGANGA EXPRESS na baadae MAJINJAH SPECIAL.










Tumeondoka CHIMBADAWA ilikuwa majira ya saa mbili na dakika arobaini. Na ilipofika saa tatu na dakika ishirini tulikuwa tayari tumeshafika  Mfinga na kupitiliza .

 Hadi tunafika mjini Iringa,gari zilizokuwa zimetutangulia mbele yetu zilikuwa ni gari tatu tuu ambazo ni MBEYA EXPRESS,HOOD na ABOOD BUS. Tukakatisha kupita njia ya mtera kuelekea Dodoma.Tulipofika Ndiuka tulikutana na basi lingine la kmpuni ya SKY LINE kutoka Dodoma kwenda Mbeya.ilikuwa tayari ni saa tano na dakika kumi na saba.

Gari yetu ilikwenda mwendo wa kasi kidogo kwani ilipofika majira ya saa sita na dakika thelathini na nne tulikuwa tumeshafika hotelini kwa ajiri ya kupata chakula, Pale tulilikuta basi la kampuni ya ANOTHER G likitokea Njombe kuelekea Dodoma nao wakipata chakula lakini wao walitutangulia kuondoka.




Baada ya hapo tuliondoka majira ya saa saba kasoro dakika kumi kuelekea mjini dodoma ambapo kwa neema ya mungu tuliwasiri mjini dodoma majira ya saa nane na nusu na tulipokelewa kwa kelele nyingi sana na miruzii miingi sana ya shangwe iliyovuta hisia za watu wote waliokuwepo stndi na maeneo ya jirani wote wakishangaa basi la dodoma kuingia muda kama ule ambapo tulikuta mabasi mengine ya kutoka Dar es salaam kuelekea Mwanza na Kigoma yalikuwa hayajafika dodoma, hivyo kuwapa nafasi abiria wa mwanza na kigoma kuweza kuendelea na safari kuelekea mikoa hiyo.

HIVYO NDIVYO SAFARI YETU YA KUTOKA MBEYA HADI DODOMA ILIVYOKUWA.
Previous
Next Post »