SUPER SAMI EXPRESS WAANZA RASMI SAFARI ZA MWANZA NA IRINGA!!!!!!!!!!!!!!




Kmpuni ya usafirishaji wa abiria yenye maskani yake kanda ya ziwa mkoani Mwanza ya SUPER SAMI EXPRESS imepanua wigo wa huduma zake kwa kuanza kutoa huduma ya usafiri katika mikoa ya Mwanza na Iringa kwa kutumia mabasi mapya na ya kisasa kutoka kampuni ya zhong tong China.

Awali kampuni hiyo ilikuwa ikitoa huduma ya usafiri katika mikoa ya Dar es salaam na Mwanza, Mwanza na Bukoba tu! Kuanza kwa safari kati ya Iringa na Mwanza umesemwa na uongozi wa kampuni hiyo kuwa ni mwanzo na muendelezo wa mpango wa kampuni kutaka kutoa huduma ya usafiri iliyo bora katika nchi nzima. SUPER SAMI EXPRESS tumejipanga kuja kufanya mapinduzi ya usafiri hapa nchini kwa kutoa huduma bora ya usafiri kwa wananchi bila kuweka matabaka.

Hii inakuwa ni kampuni ya kwanza kufanya safari za Mwanza kwenda Iringa kupitia Dodoma na Mtera tangu barabara ya kuunganisha mikoa ya Iringa na Dodoma ianze kujengwa kwa kiwango cha lami!

HAYA NDIYO BAADHI YA MABASI YA KAMPUNI YA SUPER SAMI AMBAYO HUFANYA SAFARI ZA IRINGA NA MWANZA.





Previous
Next Post »