Kampuni ya usafirishaji abiria na vifurushi katika mikoa ya Dar es
salaam na Mbeya ya TSK SAFARI LIMITED imeweka bayana mpango wake wa
kuendelea kuboresha na kupanua wigo wa huduma zake kwa kampuni hiyo
kuongeza njia mbili ambazo mwanzo haikiuwa ikizifanya. Lengo la kuanza
kutoa huduma katika njia hizo ni kulingana na hali ya usafiri katika
baadhi ya njia hizo kuwa ni wa kusuasua kwa huduma zinazotolewa na
kampuni zilizopo na pia huduma hizo kutokuwa na ubora unaomfaa abiria.
Aidha chanzo chetu cha habari hizi kimetuweka wazi kuwa njia hizo zilizoongezwa ni mbili ambazo ni MBEYA - ARUSHA na DAR ES SALAAM - ARUSHA.
Kinaendelea kubainisha kuwa katika kufanikisha mpango huo wa kupanua wigo wa huduma za kampuni hiyo, tayari basi SITA mpya kabisa aina ya VOLVO zimekwishafika bandarini na zinasubiri kukamilika kwa taratibu ili ziweze kuingia njiani.Basi hizo ambazo ni kwa ajiri ya safari hizo,ni Full luxury, pia ni front engine( injini ya mbele) ambazo zimetengenezwa kulingana na mazingira na umbali husika.
Hapo awali kampuni hii ya TSK ilikuwa na jumla ya mabasi MATANO na ilikuwa ikihudumia njia MBILI tuu ambazo ni DAR - MBEYA, DAR - TUNDUMA kila siku.