SKY LINE YAANZA SAFARI ZA MBEYA NA DODOMA!!!!!!!!!!!!!!


BASI LA SKY LINE


Kwa muda kidogo kumekuwa na hali ngumu ya usafiri katika mikoa ya Mbeya na Dodoma kutokana na kuwepo kwa  uhaba wa kampuni za mabasi ambazo hufanya safar zake katika mikoa hiyo. Kwa zaidi ya mwaka sasa mikoa hii imekuwa ikihudumiwa na kampuni tatu tuu za mabasi ambazo ni SUMRY HIGH CLASS,HOOD COMPANY LIMITED na UPENDO BUS TRAVELLERS.

Hata hivyo kampuni mbili zilisimama na kusababisha uhaba na shida sana kwa wasafiri ambao wamekuwa na hitaji la kusafiri katika mikoa hii miwili ambazo ni SUMRY na HOOD BUS, na kuiachia UPENDO peke yake jukumu hilo la kuhudumia mikoa hiyo.

Kwa kuangalia hitaji la wakazi wa mikoa hiyo,kampuni ya SKY LINE BUS,imeamua kuanza rasmi kutoa huduma ya usafiri kwa kutoa mabasi mawili kila siku kwenda na kurudi katika kuhakikisha kuwa huduma ya usafiri katika mikoa hiyo mi wili ina imarika na kuwa si ya kusuasua kama ilivyokuwa wali. Hii pia ni neema kwa wakazi wa mikoa hiyo kwani kwa sasa wana uwezo wa kusafiri kwa muda wa masaa nane hadi tisa tuu na kukamilisha safari yao ambapo ni tofauti na wali kwani walikuwa wakitumia zaidi ya masaa kumi na moja hadi kumi na tatu kukamilisha safari yao!

SHUKURANI ZIENDE KWA SKY LINE BUS NA WENGINE WATAKAOFUATA NYAYO HOZO!!!!

 Basi la SKY LINE likiwa Mbeya Bus Terminal baada ya kuwasili kutokea mjini dodoma majira ya saa 8.45 mchana.

 Basi la SKY LINE likiwa hotelini Mtera kwa ajiri ya abiria kujipatia chakula kwa ajiri ya safari yao ya kueleka mjini Dodoma.

 Mabasi ya kampuni ya Another G linalofanya safari za Songea na Dodoma na SKY LINE yakiwa yamepaki hotelini mtera kwa ajiri ya abiria wao kupata chakula kabla ya kuendelea na safari.

 Baadhi ya wauzaji wa vyakula na matunda katika hoteli ya hiyo.

Nyama ya mbuzi ndiyo nyama inayopatikana kwa wingi na kuuzwa zaidi katika hoteli hii japo pia kuna samaki na kuku pia!

Previous
Next Post »