WASAFIRISHAJI PELEKENI MABASI MKOANI RUKWA NA KATAVI

Nijambo la kufurahia na kuipongeza serikali kwa kazi nzuri iliyoifanya na inavyozidi kufanya kwenye mradi wa utengenezaji wa barabara inayoonganisha mikoa ya Mbeya na Rukwa hususani katika wilaya ya Sumbawanga kwa kiwango cha lami kwa sasa zimebaki kilomita chahce sana ili barabara hiyo iweze kukamilika na hivyo kuleta changamoto kubwa sana kwa wasafiri na wasafirishaji walioonja kero ya vumbi tangu nchi ilivyopata uhuru pia hii itakuwa fursa nzuri sana kwa wafanyabiashara ambao hutegemea usafiri haswa wa mabasi na mpaka sasa wapo wazalendo au kampuni mbalimbali kubwa za usafirishaji ambazo tayari zimeshaanza kutoa huduma za usafirishaji mikoani humo kwa upande wa mbeya kwenda sumbawanga kuna mabasi kama Sumry high class,Mbeya express,Ngomuo trans,Ndenjela coach,Shalom express,Mwasha exprss,Ngongis,Katavi tours,Ruchoro express pamoja na God willing coach.Pia kuna usafiri wa Noah ambazo huanzia safari tunduma mpaka sumbawanga .vile vile hizi ni baadhi ya kampuni ambazo zimeshika tenda za ujenzi wa barabara hizo
SUMBAWANGA-LAELA(95.31KM)
Sehem hii imejengwa na kampuni ya Aarsleff Bam International Joint Venture V.O.F kutoka kutoka Denmark na uholanzi kwa gharama ya dola za kimarekanimilioni 97chini ya mhandisi mshauri Egis BCEOM International kutoka ufaransa
LAELA-IKANA(64.2KM)
Sehemu hii imejengwa na kampuni ya China New Era International Corporationkutoka china kwa gharama ya shilingi bilioni76.1
IKANA-TUNDUMA(63.7KM)
Sehemu hii imejengwa na kampuni ya Consolidated ContractorsGroupS.A(Offshore)
(ccc)kutoka Ugiriki kwa gharama ya shilingi bilioni 82.5.

Vile vile kuna miradi mingine ya ujenzi wa barabara zipo zilizo kamimilika na amabazo bado hazijakamilika kama vile sumbawanga-namanyere na kizi kibaoni (245km) sumbawanga kanazi (75km) sumbawanga -Matai-kasanga port (112km) chini ni baadhi ya kampuni za mabasi ambazo tayari zinafanya huduma ya usafirishaji mkoani humo.











Previous
Next Post »