KAMPUNI ZA MABASI TANZANIA ZATAKIWA KUIGA MIFANO KUTOKA KWA KAMPUNI ZA KENYA!!!



Wadau wanaotumia usafiri wa mabasi nchini Tanzania kwa safari za ndani na nje ya nchi wamezitaka kampuni za mabasi za nchini kuiga mifano ya wenzao wa kampuni za mabasi za Kenya kwa kuziendesha kampuni hizo kwa kulingana na nyakati husika na ambazo ni nyakati za Digital kwa kuwa na taratibu ambazo ni za kisasa katika masuala mazima ya ushushaji wa abiria,upakiaji wa abiria na mizigo, ufanyaji wa booking na pia kwa mahitaji ya ukodishwaji wa mabasi yao kutumika kwa shughuli mbalimbali









Pia wadau hao wameenda mbali kwa kusema kuwa wanashangaa kuwa hadi leo kampuni za Tanzania zinakosa kuwa na tovuti (website) kwa ajiri ya kuweka Taarifa muhimu (informations)ambazo kwa namna moja au nyingine zinakuwa ni msaada kwa abiria hasa walio mbali kuweza kujua namna ya kukata tiketi au kufanya booking na mambo mengine yanayohusu usafirishaji.

Wadau hao wametoa maoni yao kuwa ni wakati sasa kwa kampuni za mabasi za Tanzania kuiga mifano kwa kuwa na mahusiano mazuri na abiria wao kwa kubadirishana nao taarifa mbalimbali zinazohusu usafiri, wamezitaka kampuni hizo angalau kuwa hata na  akaunti au kurasa(page) katika mitandao ya kijamii kama vile Facebook,Whatsapp twitter n.k ili kuweza kuwafikia watu wengi na kuwapa abiria wao nafasi ya kutoa maoni moja kwa moja na vile vile akaunti hizo ni lazima ziwe na mtu anayeziongoza kwa kuchukua maoni na kuyafikisha kwa uongozi kwa ajiri ya kufanyiwa kazi. Akiongea na mwandishi wetu mdau wa usafiri nchini ambaye ni mfanya kazi katika moja ya kampuni za mabasi hapa nchini ambaye hakutaka jina lake liandikwe alisikika akisema hivi "Imekuwa ni jambo kawaida kabisa kwa makampuni ya mabasi tanzania kujitahidi kuleta mabasi mazuri yenye huduma nzuri lakini tatizo moja kubwa walilonalo wamiliki wa mabasi yetu haya ni kukosa kuyaendesha kidigital,  inakuwa ni vigumu sana kwa msafiri wa kampuni fulani kushindwa kuwasiliana na kampuni hiyo pindi anapohitaji huduma mfano booking hata kutoa maoni.si hayo tu hata matangazo ya mabasi yao imekuwa ni vigumu sana kuyafanya" ."Hivi ni kweli kuwa kampuni ya Mabasi inashindwa kuanzisha website? kama website ni tatizo je imeshindwa kujiunga na mitandao ya kijamii?"

Nimejaribu kufuatilia nikakuta kampuni nyingi Tanzania hazina mawasiliano yoyote hata mawasiliano yaliyowekwa ni mfu.mfano nimetembelea faceebook za kampuni kadhaa za mabasi hapa bongo lakini account zao ni sawa na bure hazitumiki waliweka kama pambo.uni kama
tofauti kabisa na kampuni za mabasi za kenya ambazo zina website na mawasiliano mengine ambayo ni hai.mfano tembelea facebook kwa makampuni kama OTANGE, THE GURDIAN,COAST AIR,MORDEN COAST,SPANISH, MASH POA TAHMEED NA MENGINE MENGI USHUHUDIE JINSI BLOG ZAO ZINAVYAFANYA KAZI  hii ni ishara tosha kuwa kenya wameamka mapema sisi bado tupo usingizini.
  
Mbali na hayo wenzetu  kampuni nyingi za kenya zina sehemu zao maalum za kupakia na kushushia abiria kinyume na makampuni ya tanzania ambayo mengi ukiwa  bus stand huwezi jua ni kibanda kipi hasa kinahusika na basi gani  kutokana na kibanda kimoja kuwa na mapambo ya maandishi ya kampuni kama kumi.TUBADILIKE 

ZIFUATAZO NI BAADHI YA TOVUTI (WEBSITE) ZA KAMPUNI ZA MABASI ZA KENYA NA PICHA KIDOGO

 http://www.coastbus.com/
 www.moderncoastexpress
 www.masheastafrica.comhttps
://www.facebook.com/TahmeedBuses 














Previous
Next Post »