BREAKING NEWS!!! KAMPUNI YA MABASI YA LEINA TOURS IMETHUBUTU SAFARI ZA DAR-MWANZA RASMI!!!


Kampuni ya mabasi ya LEINA TOUR iliyokuwa ikifanya safari za Dar es salaam na Kahama mkoani Shinyanga na kujizolea umaarufu mkubwa sana kwa watumiaji wa usafiri wa mabasi katika njia hiyo kwa kuwa na kawaida ya kufika mapema na kuwapiku wengine, imeamua kutanua wigo wa huduma zake rasmi kwa kuongeza njia za safari zake kwa kuanza safari za Dar es salaam na Mwanza.

Kampuni hiyo ya LEINA TOUR mwanzoni mwa mwezi huu ilitangaza kuwa inatarajia kuanza safari katika njia hiyo na kuwafanya abiria wake wakiisubiri kwa hamu kubwa na shauku sana,kwa sasa imetimiza ahadi yake hiyo. Na katika kufanikisha hilo,kampuni ya LEINA TOUR imenunua basi mpya kabisaa ambayo itasaidiana na nyingine iliyokuwa ikisumbua katika njia ya kahama na Dar katika kutoa huduma.

SISI KAMA TANZANIA BOUND BUSES, TUNAITAKIA KHERI KATIKA KUHUDUMIA WADAU WETU WOTE WA NJIA HIYO KWA KADRI YA UWEZO WAO, NA PIA TUNAISHUKURU KWA KUENDELEZA USHINDANI WA KIBIASHARA AMBAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE UTASAIDIA KATIKA KUBORESHA USAFIRI.







Previous
Next Post »