Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mh.Said Meck Sadick ameitaka mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu SUMATRA kuanza utaratibu wa kuyafanyia fumigation ( kuyapulizia) dawa mabasi yote yanayotoka na kuingia jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwalinda abiria na kupambana na Mbu wanaoneza ugonjwa wa dengue ambao umeonekana kuwa ni tishio katika muda mfupi tokea ulipogundulika jijini Da es salaam katika hospitali ya tafa ya muhimbili ulipochukua maisha ya Dkt Bingwa wa magonjwa ya akili nchini, Gilbert Buberwa katika hospitali..
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh,Said Meck Sadick
Katika kutekeleza agizo hilo la mheshimiwa Meck Sadick ambalo lianatarajiwa kufanyika ndani ya wiki moja, zoezi hilo linatarajiwa kuhusisha mabasi zaidi ya 600 ambayo huingia na kutoka katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi za jirani na Tanzania kama vile Rwanda, Burundi, Uganda,Kenya,Zambia,Malawi na msumbiji na pia ameongeza kuwa gharama hizo za fumigation zinatakiwa zilipwe na wamiliki wa mabasi. Hivyo amewaomba pia wamiliki wa mabasi wote kwa pamoja kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kufanikisha zoezi hilo.
TAARIFA KWA WOTE,NI MUHIMU ZINGATIA NA MSHAURI MWENZIO!!!
Iwapo itatokea una kila dalili za homa ya dengue, dawa ya kukimbilia kwanza ni Panadol; inashauriwa usimeze KABISA Diclopar wala Diclofenac.
Iwapo utameza dawa hizi, utakuwa kwenye uwezekano mkubwa wa kupoteza maisha!!! Upatapo taarifa hii mjuze na mwenzio.........
Imetolewa na Wizara ya Afya!.