KIPANDE HIKI NI KERO NA SHIDA KUBWA KWA WASAFIRI WA MIKOA YA KUSINI!!!!!!!!!!!!!!


Taarifa kamili ni kuwa kuna kipande cha kilometa kama12 hivi hakina lami na wala mkandarasi hapitishi grader kama ilivyokuwa zamani, hamna diversion ni kama barabara ya kuelekea kijijini hamna jitihada zozote, kwan mkandaras amepak vifaa vyote kwa madai inavyosemekana anaidai serikali. Unajua niligundua tofauti nilipoona mbona vifaa vya mkandarasi havionekani na wala hamna tamko la Serikali kumuhusu mkandarasi huyo. Najua mh Magufuli angetoa tamko lakini yuko kimya. Ukipita leo kipande kile utazani ni barabara ya Wilaya tu, mkandarasi kajiweka pembeni, hata hicho kijiko kimoja kibovu bovu hivi kilikuja baadae nakimsing kilielemewa. Kiutaratibu mkandarasi anatakiwa afanye barabara ipitike, lakin kwa sasa hafanyi chochote cha maana

Malori na Mabasi yakiwa kwenye msururu mrefu mara baada ya kushindwa kuendelea na safari kwa takribani masaa zaidi ya nane katika eneo la Manzese lililopo Kilwa barabara ya Dar Es salaam kuelekea Mtwara hapo jana kutokana na eneo hilo kuharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea magari zaidi ya mia kukwama


Baadhi ya wasafiri kwenye mabasi yaendayo Dar Es Salaam kutoka Mtwara, Lindi na Kilwa na yale yatokayo Jijini Dar Es Salaam kuekelea mikoa ya Kusini wakiwa wamesimama kushuhudia juhudi zinazofanya na vijana wa eneo la Manzese na baadhi ya madereva wa malori na mabasi pamoja na abiria kuhakikisha wanasaidia magari kuvuka ili kuweza kuendelea na safari zao.


Wasafiri na wakazi wa Eneo la Manzese wakishuhudia greda lililofika kwaajili ya kusaidia kusawazisha eneo hilo na kutoa magari yaliyonasa kutokana na eneo hilo kujaa maji na tope zito yaliyosababisha magari kukwama kwa takribani masaa zaidi ya nane hapo jana.


Mabasi yatokeayo Mikoa ya Kusini kuelekea Bara yakiwa yamekwama katika eneo la Manzese - Kilwa kutokana na barabara kuwa mbovu katika eneo hilo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea kusababisha magari zaidi ya mia kunasa na kutoendelea na safari zao kwa zaidi ya masaa nane.



Greda likiondoa tope na kusawazisha eneo hilo ambalo lilileta usumbufu mkubwa sana kwa watumiaji wa barabara ya Dar Mtwara na kupelekea magari zaidi ya mia kukwama katika eneo hilo lililoaharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.




Malori yakiwa kwenye msururu.

SOURCE. JAMII FORUM
Previous
Next Post »