BAADHI YA MABASI YAENDAYO MIKOANI YASHINDWA KUFANYA SAFARI KWA KUTOPULIZIWA DAWA!!!!


Baada ya zoezi la kufanya fumigation Mabasi yaendayo mikoani na nchi za jirani kukamilika jana,tarehe22/5/2014 leo asubuhi katika stendi ya mabasi yaendayo mikoani (UBT) kulikua na zoezi la ukaguzi wa mabsi hayo kuangalia kama yametii agizo lilitolewa na mkuu wa mkoa wa dar es salam siku chache zilizopita.

Zoezi hilo lilisimamiwa na jeshi la polisi,sumatra na watu wa afya wa jiji. Katika ukaguzi huo imeonesha kuwa kampuni nyingi za usafirishaji zimetii agizo hilo wakati baaadhi ya kampuni zikiwa bado hazijatimiza agizo hilo, baadhi ya mabasi yaliyokamatwa ni pamoja na Leina Tours, super sami, Mapanda express, Adventure, Champion Coach, Kwa wapendwa, Taqwa, Sumry, Al hushoolum na
lampard express.

Wahusika wa mabasi hayo wamelilalamikia zoezi hilo kuwa limetwaliwa na kasoro nyingi zikiwemo kutokupewa stika za utambulisho kwa mabasi ambayo tayari yamekwishafanyiwa upuliziaji wa dawa hiyo, pia kutokuwepo kwa taarifa maalumu kwa wamiliki wa mabasi kuwa zoezi litakuwa ni la kulipia au ni bure kama baadhi ya wafanyakazi katika mabasi hayo walivyodai.

Akiongea na TANZANIA BOUND BUSES, agent wa basi la kampuni ya  champion alielezea kwa kuonesha kushangazwa na zoezi hilo  kwa kusema "ninashangaa, wengi wetu tumeshafanya zoezi hili la fumigation lakini hatukupewa stika ya kutembea nayo kwenye basi, vilevile alisema zoezi hili mwanzoni walitangaza ni bure sasa tunashangaa wanatucharge tsh 65,000/= kwa kila basi".

Zoezi la fumigation kwenye mabasi yaendayo mikoani na nchi za jirani ni agizo ambalo lilitolewa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni jitihada za haraka za kupambana na ugonjwa hatari wa DENGUE uliolipuka siku za hivi karibuni ukianzia mkoani humo na kuchukua uhai wa watu kadhaa akiwamo Daktari bingwa katika hospitali yaa taifa ya Muhimbili.

TAZAMA MABASI YAKIKAGULIWA KATIKA STENDI KUU YA MABASI YAENDAYO MIKOANI NA NCHI JIRANI UBUNGO!





Previous
Next Post »