BREAKING NEWS!!!! SUPER SAMI KUSAFIRI UMBALI WA KILOMITA ZAIDI YA KM1350 MWANZA - TUNDUMA!!


Kampuni ya usafiri ya SUPER SAMI EXPRESS yenye maskani yake jijini Mwanza, imeanza majaribio ya safari yake mpya ya Mwanza hadi Tunduma. SUPER SAMI EXPRESS imeanza majaribio ya safari hiyo juzi kwa kuruhusu basi moja aina ya YUTONG yenye injini ya SCANIA kuondoka jijini Mwanza na kuelekea mjini Tunduma mpakani mwa Tanzania na Zambia. Basi hilo kwa mara ya kwanza liliondoka Mwanza saa kumi na mbili alfajiri na lilitegemewa kuwasili mjini Tunduma majira ya kati ya  saa sita hadi saa saba na hiyo ni kutokana na umbali wa safari hiyo.
 HILI NDIYO BASI LILILOFANYA SAFARI YA MWANZA - TUNDUMA JUZI.

Hii ni mara ya pili kufanya majaribio ya safari kama hili ya kwanza likiwa ni lile la safari za kati ya  Musoma na Dodoma ambayo wameisitisha na kutafuta njia nyingine. Kimsingi kampuni hii inajitahidi kwa kuleta changamoto katika usafiri kwani kati ya mabasi yake yote saba,manne ni mapya na ya kisasa kabisa kutoka kampuni ya ZHONGTONG CHINA na pia wana mpango wa kuingiza basi mpya kabisa aina ya ZHONGTONG new model hivi karibuni.!

TAZAMA BAADHI YA MABASI YA KAMPUNI HIYO HAPA CHINI!!  











Previous
Next Post »