Hiki ndicho kilichosemwa na meneja wa kampuni ya super feo bw.Sengo juu ya basi la kampuni yake kudaiwa kuungua moto na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.
Kwanza Kampuni ya Super Feo Express imesikitishwa sana na taarifa hizi za upotoshaji. Tunajua hizi ni mbinu za watu wanaotaka kuchafua jina na biashara yetu. Ukweli ni kwamba basi halikuteketea kwa moto kama ilivyoandikwa na gazeti la Majira. Kulitokea hitilafu ya kuvuja kwa mafuta yaliyodondokea kwenye bomba la joto kali la kutolea moshi na hivyo wakati mafuta yanaungua ukafuka moshi uliosababisha taharuki kwa abiria. Dereva wetu alisimamisha gari na abiria wote walishuka salama. Basi halikuteketea wala kuungua moto kama ilivyoandika. Na hata baada ya abiria kushuka basi letu lingeweza kuendelea na safari lakini kwa sababu ya hali ya taharuki na hofu na pia tukizingatia kampuni yetu ina mabasi mengi kwenye vituo mbalimbali tuliamua kuchukua basi jingine pale Iringa na abiria wakaendelea na safari yao kama kawaida. Kwa hiyo nachukua nafasi hii kuwatoa hofu wananchi na wateja wetu kwamba taarifa hizi za kuteketea kwa basi la Super Feo sio kweli na wazipuuze. Daima kampuni yetu inatumia mabasi mazuri, bora na salama kwa abiria. Mabasi yetu yanafanyiwa matengenezo ya uhakika na kufungwa vipuri vya uhakika kila inapohotajika. Zaidi ya hapo Super Feo kila siku ina hakikisha wananchi wanapata kilicho bora. Na kwa sasa timu ya wataalamu inakamilisha mambo mengine mazuri kwa ajili ya kuboresha huduma zetu.