MZIMU WA AJALI LINI UTAKOMA ??? ULIISIKIA HIIII? SOMA CHANZO CHAKE!!



Mzimu wa ajali za barabarani umeendelea kuliandama taifa la Tanzania kadiri siku zinavyozidi kwenda, Tatizo hili la ajali za barabarani limekuwa likihusishwa na mambo mengi yakiwemo ya mwendokasi, uzembe wa madereva, ukaidi, dharau, na ushirikina .

Juzi huko mkoani Morogoro watu zaidi ya 50 wamenusurika kifo na wengine 15 wamejeruhiwa vibaya baada ya kutokea kwa ajali iliyoyahusisha mabasi ya abiria ya mikoani ya kampuni za ABOOD BUS T 830AWY  linalofanya safari zake kati ya Morogoro na Dar es salaam na basi la TAK-BIR linalofanya safari zake kati ya mkoa wa Dar es salaam na Geita. Ajli hiyo ilitokea katika maeneo ya kijiji cha Lubungo mikese mokoani Morogoro ,

Majeruhi na walionusurika katika ajali hiyo walielezea kuwa chanzo cha ajli hiyo ni mwendokasi wa basi la TAK-BIR ambao ulimfanya dereva ashindwe kulimudu basi lake na kupelekea kuligonga basi la ABOOD kwa nyuma na kusababisha maafa hayo. walizidi kusema kuwa na baada ya ajali hiyo, dereva wa basi la TAK-BIR alikimbia kusikojulikana.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paulo alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwaomba madereva wa magari hasa mabasi ya mikoani kuwa makini na kutoendesha magari ya kwa mwendo kasi kiasi cha kushindwa kuyamudupindi itokeapo dharula kama hiyo!
Previous
Next Post »