ILYANA 7, ILYANA 8 NA ILYANA 9!!!! UJIO MPYA WA OTA HIGH CLASS, BUKOBA RAHA KWENU!




Huu ndiyo ujio mpya wa kampuni ya OTA HIGH CLASS , ni kampuni mojawapo kati ya kampuni zinazotoa huduma zake katika mikoa ya Dar es salaam na Bukoba, Ni kampuni iliyodhamiria kutoa huduma bora kila kona ya nchi ya Tanzania kwa kutumia basi mpya kabisa na za kisasa ili kuweza kukidhi haja za wa Tanzania walio wengi. N a kwa kuanzia, kampuni ya OTA HIGH CLASS imeingiza basi mpya TATU aina ya ZHONGTONG CLIMBER kwa lengo la kufanikisha azma yao ya kutoa huduma bora kabisa katika sekta ya usafiri.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hii mr. Jerry Jerry akiongea na mwandishi wetu wa blog hii ametuambia kuwa kwa sasa wana mpango wa kuifanya kampuni ya OTA kuwa ni moja kati ya kampuni za mfano hapa nchini kwa kuwa na huduma zilizo bora na zenye kukidhi viwango na thamani ya nauli anayoitoa mteja,ndiyo maana hawana utaratibu wa kununua basi ambazo zimekwisha kutumika na kampuni nyingine kabla yao isipokuwa basi mpya kabisa!!

TAZAMA BAADHI YA BASI ZAO MPYA!






Previous
Next Post »