HIZI NDIYO BARABARA ZETU SISI TULIOPO TANGANYIKA MVUA IKINYESHA!!!!

Hizi ndiyo barabara za mikoa ambayo inaonekana kusahaulika sana na serikali na mingine kufikia hatua ya kuiita kuwa ni mikoa ya Tanganyika na si ya Tanzania. Barabara hizi kipindi cha mvua za masika zimekuwa ni mateso sana kwa wasafiri wa kutoka wilaya na mikoa hiyo kwani wengine wamekuwa wakitumia hadi siku mbili kwa safari ya msaa 3 kwa sababu ya kuwepo kwa tope linalofanya gari kukwama na kushindwa kutembea kabisa!

Katika mikoa hiyo, kwa wae abiria wanaosafiri ikifika kipindi hiki cha masika, huwalazimu kusafiri wakiwa na mikate na juice ambayo huwa si zawadi kwa wapendwa wao wanaokwenda kuwasalimia au walikotoka, bali ni kwa ajili ya chakula njiani kwa sababu suala la kulala njiani imekuwa ni kawaida sana kwao na wao wameshaichukulia kama ni hali ya kawaida kwa sababu wameanza kulalamika miaka mingi juu ya barabara hizo lakini hakuna kinachofanyika.

Hivyo basi wakazi wa mikoa na wilaya hizo, wanazidi kuiomba na kuisisitiza serikali kuwa wanahitaji uboreshaji wa miundombinu ya barabara ili na wao waweze kufurahia maendeleo yaliopo katika sekta ya usafiri, na pia waweze kunufaika na rasilimali zataifa hili kwani mambo mengi yanakwama kwa sababu ya kuwa na miundombinu mibovu kama hii!

Baadhi ya maeneo na wilaya hizo ni mikoa ya KATAVI-barabara za kuingia mkoani humo kutokea TABORA, RUKWA/SUMBAWANGA,KIGOMA, pia Ifakara na kirombelo mkoani morogoro,Idete mkoani IRINGA, Sikonge kwenda Tabora,Tabora kwenda Chunya, Hizo ni baadhi tuu, zipo nyingi sana ambazo zimesahaulika kabisa, hivyo tunaiomba serikali izitazame barabara hizi kwa sababu pia ni muhimu sana kwa wakazi wa maeneo haya!







Previous
Next Post »