BREAKING NEWS!! MADEREVA WA MABASI WAGEUKA DILI KAMA ALMASI!!!!


Katika hali isiyo ya kawaida, madereva wa mabasi nchini Tanzania wamegeuka na kuwa dili zaidi ya Almasi na thamani yake! Madereva hao wa mabasi wamekuwa ni dili kubwa sana polisi wa vikosi vya usalama barabarani kwani wamekuwa wakiwawinda kama kwa udi na uvumba kiasi cha madereva kukosa amani na uhuru katika Kazi yao hiyo!


TANZANIA BOUND BUSES ilipoongea na baadhi ya madereva Wa mabasi ya mikoani kuhusu wao kugeuka na kuwa dili kwa askali Wa usalama barabarani wamekili kuwa ni ukweli kuwa wao wamekuwa ni dili kuliko hata ajira za utumishi kwani wanawidwa sana kiasi cha kukosa amani katika Kazi na pia kinawafanya wa concentrate katika tochi zaidi kuliko vitu vingine vya msingi katika kazi zao kama vile timetable zao!


Wamezidi kusema kuwa na kwa sasa wakikamatwa kwa tochi malipo ni 20000 hadi 50000 bila notification kwa maana kuwa hizo wanafaidika wao askali waliokukamata na pia unaenda lockup siku 14 na leseni unanyang'anywa pia unapandishwa mahakamani likiwa ni agizo kutoka kwa kamanda Wa kikosi cha usalama barabarani lengo ikiwa ni kujaribu kupunguza ajali!
Katika kuzingatia usawa kwa suala hili, TBB ilijaribu kuzungumza na baadhi ya askari wa usalama barabarani ambao walikataa kutoa ushirikiano na kudai kuwa wao si wasemaji na hawana ruhusa kuongelea hayo mambo




Previous
Next Post »