BREAKING NEWS!! HAYA NDIYO MABASI HUTAKIWI KUPANDA KWA USALAMA WA MAISHA YAKO!!!!!!


Kumekuwa na ongezeko la wimbi kubwa la ajali hapa nchini Tanzania ambazo zimekuwa zimekwisha gharimu maisha ya wa Tanzania takribani 800 katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari na Machi mwaka huu. Kuzidi kuongezeka kwa wimbi hili la ajali nchini Tanzania kumefanya watu wengi wakiwemo wasomi na wataalamu kuumiza vichwa ni namna gani ya kuweza kupunguza au kukomesha kabisa wimbi hili la ajali ambazo nyingi sana zimekuwa ni za uzembe na si za lazima kutokea.
Katika upande wa Traffic , wao walijaribu kutoa maelekezo ya utekelezwaji wa sheria ya mwendokasi wa 80kph ambao ulionekana kuwa ni kero kwa madereva na pia kwa abiria ambao wameonekana kupendelea zaidi mwendo kasi kwa lengo la kutaka kuwahi kufika maeneo yao tarajiwa. Pia walifanya utekelezaji wa sheria ya refresher course baada le muda wa leseni kuisha, sheria hii ilileta mkanganyiko na mgogoro mkubwa sana hadi kufikia madereva baadhi kugoma na  kuwashinikiza madereva wengine kutoendesha magari hadi itakapotolewa sheria hiyo ili wasiweze kurudi masomoni tena kujiendeleza katika taalma zo!

Mimi nikiwa kama mdau katika sekta hii ya mabasi, nimejaribu kufanya utafiti wangu kwa kiasi fulani ili kuweza kujua na kupata kufahamu ni kitu gani zaidi aabiria ambao wanahisi kuwa wao wakifanya basi wataweza kupunguza wimbi hili la ajali nchini na upotevu wa nguvu kazi, nao baadhi walitamka kuwa kwa usalama zidi, ni vyema kutopanda mabasi haya,;
  1. Basi linalokwenda mwendo kasi kupindukia, Hii ni kwa sababu, watu wengi hawajui kuwa kadiri mwendokasi unavyozidi katika basi, uwezekano wa ajali kutokea unaongezeka pia.Hivyo basi likiwa mwendokasi sana ajali huweza kutokea kirahisi sana na kuikwepa au kuiepuka ni vigumu.
  2. Mabasi ambayo ni mabovu mabovu, Mabasi haya huwa asilimia kubwa sana ya kusababisha ajali tena ni zaidi ya yale niliyoyataja hapo katika nambari moja endapo derva hatokuwa makini zaidi kwa usiriazi wa chombo chake.
  3. Mabasi yenye madereva walevi, Mabasi yenye kuendeshwa na madereva wanaokuwa na mazoea ya kutumia vilevi pindi wanapoendesha  kama vile viroba, bangi, konyagi, bia na mirungi, hivi huwafanya mabereva hao wasiweze kuwa na hofu ya kutokea kwa ajali kwa sababu anakuwa ameshatokwa na fahamu na vilevi husika ndiyo vinavyomuongoza katika kuendesha basi hilo
  4. Mabasi yanayosifika kwa mbio zaidi katika mitandao ya kijamii, Mabasi haya mengi  yamekuwa yakisifika kwa mbio katika mitandao ya kijamii, na humo pia kuna madereva ambao wamekuwa wakiona wanavyosifiwa , hivyo wanaongeza juhudi katika kufanya vitendo hatarishi pindi waendeshapo mabasi yao ili tu wapate kusifiwa zidi ya wengine katika mitandao ya kijamii na kufanya uwezekano wa ajri kutokea kuwa mkubwa sana!
  5. Mabasi ambayo hayawathamini watumiaji wengine wa barabara! Kumekuwa na ongezeko kubwa la kampuni za mabasi nchini ambalo pia limepelekea watumiaji wengine wa barabara wakiwemo wa mgari binafsi kutoheshimiwa na kutambulika na madereva hawa wa mabasi ambao wengine wamekuwa wkidiriki hata kuwapiga vikumbo na kuwasababishia ajali au kusababisha ajali za kizembe!
Pia kumekuwa na mitazamo mingi sana ikiwemo ya kuhusisha ajali hizi na masuala ya ushirikina, na baadhi wengine wameenda mbali zaidi na kufikia hatua ya kuhusisha na masuala ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaotaajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu!
Previous
Next Post »