ETI HII NDIYO SABABU YA MIGOMO YA MADEREVA !!!!!!


Sheria hiyo ni mojawapo ya kanuni au sheria ndogo ndogo zilizotungwa chini ya Sheria ya Usalama Barabarani( Road Traffic Act, cap.38), ambayo inaitwa THE ROAD TRAFFIC (EXAMINATION AND RE-TESTING OF DRIVERS) REGULATIONS, 2015; GN.31/2015.
Kifungu4 cha kanuni hiyo, kinamtaka mtu yeyote ambaye anataka kupanda daraja la leseni yake toka lile alilokuwapo kwenda kusomea kwanza daraja hilo ndipo apeleke maombi ya kupandishwa daraja, ajaribiwe ndipo apewe leseni ya daraja jipya;


Pili, Kifungu hicho kinamtaka dereva yeyote mwenye leseni daraja E,C3,C2,C1 na C kabla ya kuhuisha leseni yake baada ya muda wa leseni hiyo kwisha kuwa amefanya yafuatayo:
(a) Awe amehudhuria mafunzo mafupi ya kujikumbusha uendeshaji na kanuni za barabarani
(b) Awe amepimwa afya yake ili kuona kama bado ana uwezo wa kiumbo na kitabibu wa kuendesha gari kwa fdaraja husika
(c) Afanyiwe majaribio tena kabla ya kupewa leseni yake hiyo mpya na baada ya kuwa amewasilisha nyaraka zilizotajwa hapo juu;

Hii ina maana kwamba dereva mwenye leseni yenye mojawapo au yote ya madaraja tajwa hapo juu atatakiwa kwenda mafunzo ya muda mfupi na kupimwa afya yake kila baada ya mika mitatu(3) kwakuwa muda wa uhai wa leseni Tanzania ni miaka mitatu (3)


Tatu, Madereva wengine wote wenye leseni za kawaida ukiacha zilizotajwa hapo juu watatakiwa kwenda kwenye mafunzo ya muda mfupi kila watakapoenda kuhuisha leseni kwa mara ya pili, yaani baada ya miaka sita tangu kupewa leseni inayoisha muda wake.
Zingatia: Sheria hii haijataja chuo ambacho mtu atakwenda kusomea, ilichosema ni chuo chochote kinachotambulika, na pia sheria hii haijataja viwango vya ada za mafunzo hayo ya muda mfupi wala muda wa mafunzo hayo.
SEHEMU YA SHERIA HIYO
4.-(1) A person holding a driving licence who intends to upgrade his licence to other classes shall undergo respective training for the class of motor vehicle he intends to drive from a recognized institution.
(2) A person holding class E or C3, C2, C1 and C driving licence, upon every renewal of his licence, shall undergo re-fresher training at a recognized institution and be examined thereafter.
(3) A person holding any class of driving licence other than classes in sub regulation (2) shall be examined at every second renewal.
(4) Where the driver under sub-regulation (2) and (3) intends to appear for the test, he shall, before such appearance, obtain and produce a medical examination report of his fitness for driving a motor vehicle from a recognized medical facility.
Mtaendelea kupata uchambuzi wa kanuni hizi kadiri ziku zinavyoenda
Previous
Next Post »