Basi la kampuni ya AIR BUS lililokuwa likitokea jijini Dar es salaam kuelekea Mkoani Tabora limepata ajari jana asubuhi majira ya saa tano katika kijiji cha belega wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya abiria 5 na kujeruhi wengine zaidi ya ishirini tofauti na ilivyoelezwa na kuripotiwa na baadhi ya blog na vyombo vingi vy habari kikiwemo kituo kimoja maarufu sana cha redio nchini.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali ambao baadhi yao walikuwemo ndani ya basi hilo, wameiambia TANZANIA BOUND BUSES kuwa basi limetoka Dar likiwa na abiria 20 na lilipofika Morogoro likaongeza abiria ambao hawakuzidi kumi na kisha kuondoka. Wakiwa njiani, dereva wa basi lao bwana Hillali ambaye alikwishawahi kuwa dereva wa basi la ALLY'S BUS alikuwa akienda mwendo wa kasi na walipofika eneo la belega dereva huyo alihamia upande wa kulia wa barabara akijaribu kulipita lori ambalo nalo lilikuwa katika mwendo wa kasi,kama zilivyokuwa taratibu za uendeshaji wa magari, unapotaka kumpita mwenzako,unalazimika kuwa mwendokasi mara mbili zaidi ya yule unayetaka kumpita,na ndivyo ilivyokuwa kwa dereva wa basi hilo.
Na katika patashika hiyo, ndipo steering rod ya basi hilo ikakatika na basi kupoteza uelekeo na kubilingita upande wa korongoni na kusababisha vifo vya abiria hao wanne na majeruhi zidi ya ishirini.
TAZAMA PICHA ZA MFANO WA STEERING ROD ILIYOKATIKA!
TAZAMA PICHA ZA AJALI HAPA CHINI
Basi hilo enzi za uhai wake maeneo ya Bahi road Dodoma!
Mmiliki wa basi hilo akipatiwa msaada wa kwanza baada kuvunjika mkono katika ajali hiyo