HIZI NDIYO BASI MPYA ZA KAMPUNI YA ABOOD!!!!



Kampuni ya usafirishaji wa abiria na mizigo nchini Tanzania ya ABOOD GROUP inayomiliki kampuni mbalimbali ikiwemo ya ABOOD BUS SERVICE imeingiza basi mpya kabisa nchini aina ya yutong F12 new model kwa ajiri ya kuendeleza utoaji wa huduma za usafiri nchini Tanzania.

Kumekuwa na taarifa mbalimbali tofauti tofauti kuhusiana na idadi kamili ya basi hizo huku wengine wakisema kuwa zipo basi 50, wengine zipo basi 12 na wengine zipo basi 15, lakini ukweli halisi wa idadi ya basi hizo bado haujawekwa wazi kwani basi hizo bado hazijaanza kutoa huduma ya usafiri kwa sababu kwa sasa zipo katika harakati za kutafutiwa vibali vya njia tofautitofauti.

TUUPOKEE UJIO HUU WA ABOOD KWA KUMUUNGA MKONO KATKA KILA NJIA ZITAKAPOPELEKWA!








Previous
Next Post »