ABIRIA WASUBIRI WANAFUNZI HEWA NDANI YA BASI ZAIDI YA MASAA MATATU MOROGORO!!!!!!

Katika hali isiyokuwa ya kawaida katika suala zima la usafiri mkoani Morogoro kutokana na ongezeko la vyombo vya usafiri, abiria zaidi ya 40 wamekaa ndani ya basi la kampuni ya GOMBE EXPEDITION namba T 143 BWU lenye kufanya safari zake kati ya mikoa ya Dar es salaam na Morogoro kwa zaidi ya masaa matatu wakisubiria wanafunzi hewa.

Abiria hao wamekaa ndani ya basi kutokea saa kumi na mbili kasoro wakiambiwa kuwa basi hilo linasubiri wanafunzi waliokuwa wakitoka shule kuelekea likizo Dar es salaam lakini kumbe ilikuwa ni kuwapotosha abiria hao ili waweze kusubiri abiria wengine kwa ajiri ya kujaza gari na kuendelea na safari. Ilipofika majira ya saa mbili na dakika ishirini na mbili usiku, basi hilo lilianza safari yake huku kukiwa akuna mwanafunzi yeyote aliyekuwa akisubiriwa amepanda.


Tabia hii imekuwa ni mazoea sana kwa mabasi makubwa amabayo yamekuwa yakifanya safari fupifupi kwani wamekuwa wakitumia kila aina ya uongo ili kutafuta abiria bila kutumia utaratibu mzuri kwa manufaa ya abiria kwani ndiyo waajiri wao. Mfano mzuri ni stendi ya mkoani Dodoma ambapo wameweka utaratibu wa abiria kuupanda basi ambalo lipo katika foleni, na kama haulitaki utapanda basi unalolitaka hata kama foleni yake liko mbali na itakubidi uvumilie tuu hadi lifikie zamu yake kuondoka.Na basi haliruhusiwi kuondoka endapo lililopo mbele yake halijajaza.

UTARATIBU HUU UKIIGWA NA STENDI NYINGINE  UTABORESHA SANA USAFIRI KAMA ILIVYOKUWA KWA DODOMA.
Previous
Next Post »