Tabia hii imeoneka kkua kadiri siku zinavyozidi kwenda kwa kuongezeka kwa kampuni nyingi za mabasi tofauti ambazo zinatumia rangi moja.Pia suala zima la kampuni moja ya mabasi kuwa na mabasi ya rangi tofautitofauti ilihali yote ni ya kampuni moja nayo inakuwa ni kero sana kwa abiria.
Baadhi ya wadau waliotoa maoni yao na kutaka majina yao kutotajwa hadharani wameongea kwa hali ya kuchukizwa na kitendo hiki huku wakiongelea miaka ya nyuma kuwa ilikuwa vizuri sana " Miaka ya tisini katika suala zima la usafiri wa mabasi ilikuwa ni rahisi sana kulijua basi hata kama liko mbali,ukishaona rangi tuu naja lile ndiyo basi langu napanda,lakini leo hii,basi hadi likusogelee tena mengine hadi likisimama kabisaausome jina ndiyo ulijue kuwa hili ni basi fulani" sasa hii ni kero sana kwa abiria hasa wale wanaopandia njiani au hata stendi kubwa na pia katika sehemu za kulia chakula au kuchimba dawa.
Wadau hao wameenda mbali kwa kusema kuwa, umefika wakati,hawa wamiliki wa mabasi/kampuni za mabasi wajarib kuwa wabunifu na kuweka utofautikati ya kampuni moja na nyingine ili kuwaondolea kero mbalimbali wanazozipata abiria kwa kuchanganya magari pindi wanapokuwa safarini.
Baadhi ya kampuni hizo ni hizi zifuatazo.
- Princes Muro,Princes Lucky,Princes Shabaha,Lucky Star, Princes Munaa na Royal Coach.
2. BEST LINE, NAJIMUNISA na SUPER SAMI
3.HAPPY NATION,HAI EXPRESS,MASTER CITY na ZUBERI
4. HAPPY NATION, NAJIMUNISA,SUPER BARAKA,HBS na KIPACHA EXP.
6.NBS CLASIC, MTOTO GEMA na MSEMO EXPRESS
HAYO NI BAADHI TU YA MABASI,ILA KUNA WENGINE WENGI SANA. POINTI YA MSINGI NI ,KAMA TANZANIA BOUND BUSES TUNATOA WITO KWA WAMILIKI WA KAMPUNI ZA MABASI KUIGA MIFANO YA BAADHI YA KAMPUNI KAMA SCANDINAVIA,ABOOD BUS,SHABIBY LINE,HOOD,KILIMANJARO EXPRESS,DAR EXPRESS NA NHINGINE ZENYE KUWA NA RANGI ZA AINA MOJA TUU.