BREAKING NEWS!! UPYA WA NDENJELA EXPRESS DAR-MBEYA ! SASA NI NDENJELA JET!!!!!!



Kampuni ya usafirishaji wa abiria nchini ya NDENJELA (ROYAL PRINCES)  inayofanya safari zake kati ya mikoa ya Dar es salaam na Mbeya , Mbeya -Sumbawanga na sehemu za jirani na mkoa wa Mbeya ,yenye makao makuu yake maeneo ya Uyole jijini Mbeya na Shekilango  jijini Dar es salaam imedhamiria kuboresha na kupandisha hadhi ya kampuni na huduma zake kwa kuleta basi mpya  na za kisasa kabisa kwa ajiri ya kutimiza dhamira hiyo.

Uongozi wa kampuni hiyo ulipozungumza na mwandishi wa blog hii, umesema kuwa huu ni mwanzo tuu na kuna mambo mazuri mengine yako njiani ambayo ni kwa ajiri ya wapenzi na wasafiri wa mabasi ya  NDENJELA EXPRESS, ila kwa kuanza zinakuja basi mbili mpya kabisa kutoka china aina ya ZHONGTONG NEW MODEL kwa ajiri ya kuhudumia abiria wetu.

Katika kuboresha huduma zaidi na kuzifanya zikidhi mahitaji ya abiria, kampuni ya NDENJELA EXPRESS ( ROYAL PRINCES) imeboresha safari za MBEYA -SUMBAWANGA kwa kupeleka basi zake za luxury aina ya YUTONG ambazo zitakuwa sikifanya safari za kwenda na kurudi kila siku.

Kwa maboresho hayo, machache,NDENJELA EXPRESS/ JET inakaribisha ,wasafirishaji wa mizigo ya aina zote,kuanzia PARCELS, na mizigo mingine yote kwa safari zake zote.

TAZAMA BASI MPYA ZA NDENJELA, NDENJELA JET.










Previous
Next Post »