Kampuni ya Dar coach (T) limited inayojishughurisha na utengenezaji wa body za mabasi nchini Tanzania, imezidi kujipatia soko la bidhaa zake kadiri siku zinavyokwenda ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Kampuni hiyo ambayo hadi sasa imekwishatengeneza body aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na bodi ya DIAMOND,CRYSTAL, kopi ya zhong tong climber, kopi ya yutong f11 na f12 zote zikiwa na injini za scania,tata na fuso , imezidi kupata soko nchi za nje Kama Burundi na Rwanda kuringana na ubora wa bidhaa zake.
Taarifa kutoka katika chanzo chetu cha habari zinasema kuwa kwa sasa kampuni inapokea order nyingi kutoka nchi hizo mbili za Rwanda na Burundi ,kuringanisha na nchi nyingine za ukanda wa afrika mashariki.
Hii ni chachu ya maendeleo kwa nchi ya Tanzania katika sekta hii ya viwanda ambayo serikali ya awamu ya tano ilikuwa ikisisitiza sana.
Changamoto kubwa ambayo imetajwa kuwa ni kikwazo sana katika shughuli hizi, ni gharama kubwa ya kodi katika uagizaji wa malighafi zinazotumika kutengenezea bodi hizo za mabasi, kiasi cha kupelekea uzarishaji kuwa Mdogo.