BASI LA NEW FORCE LAPATA AJALI MKOANI NJOMBE NA KUUA!!!!

Basi la kampuni ya usafirishaji abiria ya NEW FORCE limepata ajali na kusababisha vifo  na majeruhi likiwa njiani kutokea DAR kuelekea mkoani SONGEA usiku huu majira  ya saa mbili usiku.

Kwa mujibu wa taarifa za awali zinasema kuwa  basi hilo limepata ajali katika kijiji  cha kifanya  lilipogongana na lori uso kwa uso na kupinduka na kusababisha vifo  na majeruhi kwa idadi ambayo bado haijawekwa wazi.

Wakati huo huo bus la kampuni ya SIMIYU EXPRESS likitokea BARIADI  mkoani SIMIYU kuelekea jijini DAR, limeligonga kwa nyuma basi la kampuni ya ZUBERI lililokuwa likitokea jijini MWANZA   kuelekea jijini DAR katika kijiji  cha ubena zomozi mkoani MOROGORO.

Taarifa za awali zinasema hakuna vifo, ila majeruhi tuu.

Endelea kuwa nasi kuzidi kupata taarifa zaidi.

Previous
Next Post »