Kampuni ya usafirishaji wa abiria na mizigo pia vifurushi(parcels) yenye maskani yake Uyole jijini Mbeya ya NDENJELA BUS SERVICE LTD ( THE ROYAL PRINCES),imedhamiria kutoa huduma zaidi ya zile zilizokuwa zikitolewa na iliokuwa kampuni maarufu ya usafirishaji nchini ya SCANDINAVIA katika sekta ya usafirishaji wa abiria na vifurushi ( parcels) ili kuweza kukidhi haja za watumiaji wa usafiri huo ambao kwa miaka mingi imekuwa ni historia kutokana na kufilisika kwa kampuni ya Scandinavia Bus Services LTD.
Akizungumzia ujio huo wa kampuni ya NDENJELA katika sekta ya usafirishaji wa abiria kwa kutoa huduma bora na salama kwa abiria, mmoja wa viongozi katika kampuni hiyo mr. PATRICK amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha abiria wao wanapata huduma inayolingana na pesa yao na zaidi watapata huduma ambayo hawakuwahi kuipata tangu kampuni ya scandinavia ilipotoweka kaika sekta ya usafirishaji na kwa mipango iliyopo,huduma zitakuwa ni zaidi ya scandinavia .
Akiendelea kufafanua zaidi mr. Patrick amebainisha huduma ambazo kwa sasa zinatolewa katika basi hizo za NDENJELA kuwa ni , VINYWAJI LAINI(SOFT DRINKS) ,BITES/VITAFUNWA(CAKES), VITAMBAA (HANDKERCHIEF), TV, AC, WIFI (INTANETI YA UHAKIKA).
TAZAMA PICHA HAPA CHINI.
Picha juu ni muhudumu wa basi la Ndenjela akisambaza dustbin kwa ajili ya kutunzia uchafu ndani ya basi!!
Huduma ya WIFI (intaneti) inapatikana bila kikomo kuanzia mwanzo wa safari yaani DSM/MBY hadi mwisho wa safari yaani MBY/DSM.
Vinywaji (soft drinks) soda na maji zikiwa tayari kwa ajili ya kugawiwa kwa abiria katika basi
Abiria wakiwa wametulia katika seats zao tayari kwa kuendelea na safari baada ya mapumziko ya dakika 10 katika stendi ya makambako!!
Muhudumu wa basi la NDENJELA akigawa mirijakwa ajili ya kunywea soda pamoja na tishu kwa ajili ya kufutia uchafu katika mikono na sehemu mbalimbali baada ya kula ndani ya basi!!
Muhudumu akigawa cake kwa abiria ndania ya basi hilo!!
Pichani juu,muhudumu huyo akiwagawia abiria vinywaji laini kwa ajiri ya kuburudika wakati wakiendelea na safari!!!