Chama cha wamiliki wa mabasi nchini TABOA kimetangaza kusitisha huduma za usafiri nchi nzima kuanzia tarehe 4/4/2017 siku ya ijumanne hadi hapo watakapotangaza tena .
Lengo la kusitisha huduma ni kujaribu kuhimiza wabunge kutopitisha smuswada wa sheria ya usafiri ambayo imeonesha udhaifu katika kipengele cha kutotenganisha makosa ya dereva na mmiliki wa bus hali inayofanya mmiliki wa basi kuadhibiwa kwa kosa la dereva wake pindi sheria hii itakapopitishwa.