AJALI YATOKEA MKOANI SHINYANGA.

Basi mali ya kampuni ya Kidia One Express inayofanya safari za kutoka jijj la Dar Es Salaam kwenda jiji la Mwanza. Limepata ajali majira ya saa 5:30 usiku katika kijiji cha Usinde kilichopo

Katika mkoa wa Shinyanga. Chanzo cha ajali hiyo ni ng'ombe waliokuwa wakivuka barabara kwa ghafla. Dereva wa basi hilo ambaye hajafahamika kwa majina Alijaribu kuwakwepa ng'ombe hao na kujikuta akigongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitoka jijini Mwanza.
Katika ajali hiyo imesababisha vifo na majeruhi waliokimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.




Previous
Next Post »