KUTOKA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII HADI KUWA KAMPUNI YA WASAFIRI TANZANIA INVESTMENT LIMITED.





Wasafiri Tanzania ni moja kati ya makundi yaliyopo katika mitandao ya kijamii yanayohusuiana na shughuli za usafiri wa abiria na mizigo. 

Siku za hivi karibuni, kundi hili limezidi kujizolea umaarufu na kuzidi kupendwa na watu wengi sana kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi kiasi cha kufikia idadi ya wafuatiliaji zaidi ya 50,000 kutoka katika nchi mbalimbali duniani na ndani ya nchi.

Katika kuboresha huduma zake kwa jamii ya wasafiri kote duniani, kundi hili liliamua kufungua akaunti katika mitandao takribani 5 mitano ya kijamii ikiwa ni pamoja na facebook, whatsapp, twitter, you tube, Instagram na Telegram. ambapo kwa ujumla wake imeweza kujikusanyia wafuatiliaji zaidi ya 50,000.

Hivi karibuni, kundi hili limefanikiwa kutamburika kisheria na kwa sheria za nchi ya Tanzania kuwa ni kampuni inayojulikana kwa jina la WASAFIRI TANZANIA INVESTMENT LIMITED (WATIL) ambayo ndani yake kutakuwa na ofisi ndogo ndogo mbalimbali ambazo zitakuwa zikifanya kazi kwa mtazamo wa kampuni.

source: WATIL
Previous
Next Post »