FURSA YA UWEKEZAJI, KAMPUNI YA WATIL YATAFUTA WAWEKEZAJI!!



Kampuni ya Wasafiri Tanazania Investment Limited (WATIL) iliyoanzishwa na vijana wa kitanzania mwaka jana mwezi wa 11 inatangaza fursa ya uwekezaji kwa wawekezaji watakokuwa tayari kuwekeza kupitia kampuni hiyo. Uongozi wa kampuni hiyo unatangaza fursa hiyo kwa wale watakaokuwa tayari kuwekeza katika kampuni hiyo kupitia miradi yake mbalimbali.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu wakati wa kipindi cha wasafiri matukio leo mchana mmoja kati ya wakurugenzi ambaye anafahamika kwa jina la Athanas Malembeka amethibitisha taarifa hizi na kuelezea zidi kuwa kwa wale wote walio tayari na wanahitaji kuwekeza, wanatakiwa kuwasiliana na uongozi wa WATIL uliopo Dar es salaam na Mbeya katika stendi kuu ya 88 kwa ajiri ya maelekezo zaidi na taratibu muhimu za kufuata ikiwamo za kisheria.

Aidha mkurugenzi huyo, alitoa wito kwa kampuni za mabasi kuweza kuitumia fursa hiyo, ili kuweza kubadirisha kampuni zao na kuzifanya zifanye kazi kisasa zaidi na kwa huduma bora kulingana na maendeleo makubwa yanayozidi kushika kasi katika sekta hii ya usafirishaji kwani kampuni ya WATIL imesheheni wataalamu wengi sana katika masuala ya biashara na marketing kwa ujumla.

Kwa mawasiliano ya kampuni na uongozi wake ni kupitia email hapa chini.

email:  winvestmentlimited@gmail.com



Previous
Next Post »