NDENJELA BUS KUANZA KUSAFIRISHA WATOTO WA UMRI CHINI YA MIAKA 18!!!


Kampuni ya usafirishaji wa abiria na vifurushi nchini ya Ndenjela yenye maskani yake Uyole jijini Mbeya inategemea kuanza kutoa huduma ya kusafirisha watoto wa umri wa chini ya miaka 18 kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine katika njia zote ambazo imekuwa ikitoa huduma za usafiri.

Akitoa taarifa hii mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo amesema kuwa wameamua kuanzisha huduma hiyo kwani kumekuwa na usumbufu sana unaowapata wazazi na walezi ambao hukaa mbali na mahali walipo watoto wao kwa madhumuni mbalimbali kama vile masomo, likizo, na kusalimia ndugu na jamaa, hivyo wazazi wengi wamekuwa wakikosa muda wa kuwafuata au kuwapeleka mahali husika kutokana na kubanwa na shughuli za ujenzi wa taifa na jamii pia.

Hivyo kwa kuzingatia hilo na kuliona umuhimu wake, Ndenjela imeamua kuanzisha huduma hiyo ili kpunguza usumbufu uliokuwa ukijitokeza kwa wazazi! Aidha mkurugenzi huyo amesema kuwa imekuwa rahisi kwao kutoa huduma hiyo kwani kampuni yake ina wahudumu wote wa kike ambao wamekuwa na uzoefu na uangalizi wa watoto kwa muda mrefu bila kuwa na shida yoyote hivyo kupitia wao watoto hawatokuwa na shida yoyote na wala kujisikia wapweke pindi wawapo safarini!

TAZAMA WAFANYAKAZI MBALI MBALI WA KAMPUNI YA NDENJELA!








Previous
Next Post »