BREAKING NEWS! KAMPUNI YA NDENJELA YAANZA RUTI YA MPANDA-S/WANGA-MBEYA-D'SALAAM!!!


Kampuni ya mabasi ya Ndenjela yenye maskani yake uyole jijini Mbeya,imedhamiria kupanua wigo wa huduma zake za kisasa za usafirishaji wa abiria kwa kuongeza ruti mpya kabisa ya kuanzia mkoani Katavi-Mpanda kuelekea mikoa ya RUKWA, MBEYA na DAR ES SALAAM.

Akizungumza na blogu hii, mkurugenzi wa kampuni hiyo Mr. PATRICK alisema kuwa uongozi wa kampuni ya Ndenjela, umefikia uamuzi huo wa kutanua wigo wa huduma zake katika mikoa hiyo tajwa hapo juu baada ya kupokea maombi mengi kutoka kwa watumiaji na abiria ya kuihitaji huduma yao kwa muda mrefu.

Alizidi kuongeza kwa kusema kuwa wameamua kupeleka huduma hiyo ikiwa na huduma zote ambazo mabasi yake ya mikoa mingine yanazitoa kwa abiria wake. Na pia mabasi yake ni mazuri na yenye kuwa na uhakika wa safari kwani yamefanyiwa uhakiki na mafundi wa kampuni yake wakishirikiana na mafundi kutoka nchi za china na japan na kuhakiki kuwa yanweza kumudu safari hiyo na katika njia ya hali zote bila kumghasi abiria kwa namna yoyote ile!

Alimalizia kwa kuwasomba wadau wote wa usafiri wachukulie kama ni changamoto katika kuendeleza sekta ya usafiri na isionekane kama ni chuki, pia amewaomba abiria na wadau wote kuipokea Ndenjela kwa kuiunga mkono kwa kutumia huduma zake.

TAZAMA BASI ZITAKAZOTUMIKA HAPO CHINI!!











Previous
Next Post »